Darasa Janja
Darasa Janja
Imewekwa: 03 August, 2024
Ndiyo, Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) inatoa huduma ya kukodisha Darasa Janja kwa walimu na wanafunzi wanaotaka kufanya mafunzo kwa njia ya masafa. Huduma hii inalenga kuboresha upatikanaji wa elimu kwa kutumia teknolojia ya kisasa, hivyo kurahisisha mchakato wa kujifunza na kufundisha hata kwa wale walioko maeneo ya mbali. Darasa Janja lina vifaa na programu zinazowezesha masomo kufanyika kwa njia ya mtandao, ikiwa ni pamoja na vitabu vya kiada vya kielektroniki, mafunzo kwa video, na mitihani ya mtandaoni.