TUMEONGEZA ENEO LA USHINDANI KATIKA SHINDANO LA NNE LA STADI ZA UFUNDISHAJI
TUMEONGEZA ENEO LA USHINDANI KATIKA SHINDANO LA NNE LA STADI ZA UFUNDISHAJI
23 February, 2026
Pakua
Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) inawaalika na kuwahamasisha walimu wanaofundisha Darasa la Awali, na Darasa la kwanza kwa Shule za Msingi, na Kidato cha kwanza kwa shule za Sekondari za Serikali zilizopo katika halmashauri zote Tanzania Bara kushiriki katika shindano la stadi za ufundishaji la nne kwa walimu wanaofundisha Darasa la awali na msingi na la pili kwa walimu wa wanaofundisha kidato cha kwanza kwa shule za sekondari katika masomo ya Physics, Mathematics, Computer Science, na Business studies, na umahiri wa Kumudu stadi za awali za kusoma na Demonstrate mastery of basic English language skills.