Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Taasisi ya Elimu Tanzania

Historia ya Taasisi

Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) ni taasisi ya Umma ndani ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia ikiwa na jukumu kuu la kutafsiri sera ya elimu nchini na kuziweka katika mitaala na program za vifaa vya kujifunzia kwa lengo la kutoa elimu bora katika ngazi za elimu ya awali, msingi, sekondari na vyuo vya ualimu. 

TET ilianzishwa kwa sheria Na. 13 ya mwaka 1963 na kuitwa Taasisi ya Elimu kikiwa kitengo ndani ya Chuo Kikuu Kishiriki cha Dar es Salaam chenye jukumu kuu la kuratibu kazi ya utoaji wa mafunzo ya ualimu katika Chuo Kikuu kishiriki cha Dar es Salaam na jitahada za Wizara ya Elimu katika kuboresha ufundishaji na ujifunzaji mashuleni na vyuo vya ualimu. 

Mnamo Julai 1970, Chuo Kikuu Kishiriki cha Dar es Salaam kilipopandishwa hadhi kuwa chuo kikuu kinachojitegemea, Taasisi ya Elimu iliendelea kuwa Kitengo ndani ya chuo hicho hadi mwaka 1975, ilipohamishiwa Wizara ya Elimu na Utamaduni ikiwa ni taasisi inayojitegemea iliyoundwa kwa sheria ya Bunge Na. 13 ya mwaka 1975. Mwaka 1987, mabadiliko ya sheria Na. 4 yaliibadilisha Taasisi ya Elimu kuwa Taasisi ya Ukuzaji Mitaala bila kubadilishwa jukumu lake la msingi.

Miaka 50 ya Taasisi ya Elimu Tanzania