Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Taasisi ya Elimu Tanzania

PROF. MKENDA AWATAKA WATANZANIA KUJIKITA KATIKA USOMAJI WA VITABU VYA NDANI

Imewekwa: 19 February, 2026
PROF. MKENDA AWATAKA WATANZANIA KUJIKITA KATIKA USOMAJI WA VITABU VYA NDANI
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Adolf Mkenda amesema ili watoto na watanzania kwa ujumla waelewe kuhusu uzalendo ni vyema wakajikita katika usomaji wa vitabu vya ndani kuliko

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Adolf Mkenda amesema ili watoto na watanzania kwa ujumla waelewe kuhusu uzalendo ni vyema wakajikita katika usomaji wa vitabu vya ndani kuliko kusoma vitabu vya nje pekee.

Akizungumza Jijini Dar es Salaam leo, Februari 17, 2026, wakati wa hafla ya uzinduzi wa vitabu vya Tuzo ya Taifa ya Mwalimu Nyerere ya Uandishi Bunifu, Profesa Mkenda amesema unatakiwa kusoma vitabu vya ndani ili uelewe utamaduni wetu.

"nimemsikia mshairi hapa akizungumzia ngoma mbalimbali ni mshairi alikuwa anaghani mashairi, anazungumzia ngoma za wazaramo huyu anaielewa bara kuliko wabara wanavyoielewa bara yenyewe" Amesema Profesa Adolf Mkenda.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) @taasisiyaelimu amesema mtu mmoja atakumbatia kitabu hivuo mtoto akisoma anakiacha na kuja kusoma mwengine ambapo uwiano wao ni kati ya vitabu 10 mpaka 8 kwa kila shule.

Miaka 50 ya Taasisi ya Elimu Tanzania