Huduma ya Maktaba
Huduma ya Maktaba
Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) inatoa huduma bora za maktaba ya vitabu kwa walimu, wanafunzi, na wadau wote wa elimu. Huduma Zitolewazo na maktaba ya TET ni pamoja na upatikanaji wa vitabu vya kiada na ziada vya elimu ya Awali, Msingi na Sekondari, majarida mbalimbali ya kielimu, taarifa ya tafiti mbalimbali za kielimu. Maktaba ya TET ipo katika mazingira tulivu na itakuwezesha kuwa na mazingira rafiki ya kujisomea na kupata huduma bora kutoka kwa wahudumu waliobobea.
Muda wa Kufungua:
1. Jumatatu hadi Ijumaa: saa 2:00 asubuhi - saa 10:00 jioni
2. Jumamosi: Saa 3: asubuhi - Saa 10: jioni
3. Jumapili na Siku za Sikukuu: Hatufungui
Karibu sana, tafadhali wasiliana nasi kupitia library@tie.go.tz