Uthibiti Ubora
UTHIBITI
UBORA
Uthibiti Ubora ni miongoni mwa majukumu ya TET, jukumu hili huhusisha
(i). Kuainisha viwango vya vifaa na nyenzo za kujifunzia
zinazotumiwa katika shule za msingi, sekondari na vyuo vya ualimu
(ii) Kuendesha mitihani kwenye
masomo kuhusu umahiri chini ya mamlaka yake na kutoa tuzo katika ngazi za astashaahda, stashahada, Shahada na tuzo nyingine zinazohusika.
(iii) Kuwezesha
miundombinu ya uzalishaji wa vitabu , vifaa na nyenzo nyingine za kufundishia.
Katika kutekeleza jukumu hili, TET hufanya tathmini ya vitabu pamoja na maudhui yaliyoandaliwa kwa njia ya kieletroniki ili kuhakikisha kuwa vifaa hviyo vimekidhi vigezo vya ubora unaohitajika na vimeandaliwa kulingana na miongozo mbalimbali kabla ya kupata Ithibati kutoka kwa Kamishina wa Elimu ambaye ndiye mwenye jukumu la kutoa ithibati kwa machapisho yaliyokidhi viwango.
Orodha ya Vitabu vya Kiada, Ziada na Machapisho Mengine yaliyofanyiwa tathmini na Kupata Ithibati