WAANDISHI BUNIFU WAASWA KUENDELEA KUWASILISHA MISWADA YAO
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mhe. Prof. Adolf Mkenda ametoa wito kwa waandishi bunifu nchini kuwasilisha miswaada yao ya kabla ya kufungwa kwa pazia la ukusanyaji wa miswaada ya Tuzo za Mwalimu Nyerere za Unadishi bunifu kwa mwaka 2026/2027.
Dirisha la kukusanya miswada hiyo linatarajiwa kiufungwa tarehe 30/11/2026 ambao baadae kamati husika ya Tuzo itakaa na kufanya uchambuzi wa waliofanikiwa kuingia kwenye hatua ya kushindana.
Mh. Mkenda ametoa wito huo leo tarehe 20/10/2026 jijini Dar es salaam wakati akizungumza kwenye uzinduzi wa kongamano la huduma za maktaba ya Taifa ambapo amesema tuzo hizo ni fursa pekee kwa waandishi bunifu nchini kuonesha uwezo wao wa kuandika maandikio ya kitanzania na baadae kujipatia fedha kutokana na Zawadi zitakozotolewa.
“Nawaomba sana waandishi wa vitabu nchini muweze kuwasilisha miswaada yenu kabla ya dirisha kufungwa tarehe 30 mwezi Novemba mwaka huu hakikisheni mnaandika maandiko yenye kuelezea mambo mazuri ikiwemo utamaduni wa kitanzania,”amesema Mhe. Mkenda.
Kwa sasa waandishi bunifu wote wanaendelea na mchakato wa uandishi na kutuma kazi zao kwa kamati husika inayoongozwa na Mwenyekiti wake, Prof. Penina Mlama.
Tuzo hizo zinashindaniwa katika vipingele vya Riwaya, Hadithi za Watoto, Ushairi na Tamthiliya ambapo washindi wake hupatikana kila tarehe 13, April ya kila mwaka katika kumuenzi ,Mwalimu Juilius Kambarage Nyerere.
Mkurugenzi wa Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) Dkt.Aneth Komba na ni mmoja wa viongozi walioshiriki katika kongamano hilo lilioanza kuanzia tarehe 19- 22-2026 katika viwanja vya mkataba kuu ya Taifa.