Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Taasisi ya Elimu Tanzania

TET NA CHILDREN IN CROSS FIRE ZASAINI MAKUBALIANO YA KUIMARISHA ELIMU YA AWALI NCHINI.

Imewekwa: 02 November, 2026
TET NA CHILDREN IN CROSS FIRE ZASAINI MAKUBALIANO YA KUIMARISHA ELIMU YA AWALI NCHINI.
TAASISI ya Elimu Tanzania (TET) imesaini hati ya makubaliano na Shirika lilolakiserikali la Children In Cross Fire yatayosaidia kuimarisha watoto wa Elimu ya Awali nchini hasa katika stadi za

TAASISI ya Elimu Tanzania (TET) imesaini hati ya makubaliano na Shirika lilolakiserikali la Children In Cross Fire yatayosaidia kuimarisha watoto wa Elimu ya Awali nchini hasa katika stadi za kusoma, kuandika na kuhesabu (KKK).

Makubaliano hayo yaliyoshuhudiwa na viongozi mbalimbali kutoka taasisi zote mbili yamesainiwa leo Oktoba 28,2026 na Mkurugenzi Mkuu wa TET Dkt. Aneth Komba pamoja na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Children In Cross Fire Bw. Craig Ferla.

Akiongea baada ya hafla hiyo fupi Dkt. Aneth Komba amesema, makubaliano hayo yamekuja wakati mwafaka, kwani Serikali kupitia Taasisi ya Elimu Tanzania inatekeleza Mkakati wa Kisayansi wa kujenga umahiri wa Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) uliozinduliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan. 

"Makubaliano haya yamekuja wakati mwafaka kabisa, wakati Serikali ya awamu ya sita na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kupitia Taasisi ya Elimu Tanzania ikiendelea na utekelezaji wa mpango mkakati wa kuimarisha stadi za kusoma, kuandika na kuhesabu,," amesema Dkt. Komba. 

Amesema, makubaliano hayo yamejikita katika kuimarisha utoaji wa elimu ya Elimu ya Awali na Elimu ya Msingi Darasa la Kwanza na la Pili, na kusisitiza kupitia makubaliano hayo TET kwa kushirikiana na Children In Cross Fire itaimarisha uandaaji wa vifaa vya kufundishia na kujifunzia ikiwemo vitabu na viongozi vya mwalimu. 

Sambamba na hilo, Dkt. Komba amesema kupitia ushirikiano huu, TET na Children In Cross Fire inataraji kuimarisha mafunzo ya Mtaala ulioboreshwa kwa walimu, Sambamba na kuandaa vifaa vya kufundishia na kujifunzia.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkazi wa Shirika lilolakiserikali la Children In Cross Fire Bw. Craig Ferla amesema, Children Cross Fire imekuwa na ushirikiano na TET kwa takribani miaka kumi katika kutekeleza uandaaji wa vifaa kazi vya kujifunzia na kufundishia sambamba na mafunzo kwa walimu katika kuboresha Elimu ya Awali na Msingi Darasa la Kwanza na la Pili. 

Amesema, uwekezaji kwenye Elimu ya Awali na Elimu ya Msingi Darasa la Kwanza na la Pili ni nguzo muhimu sana katika safari ya ukuaji wa Elimu kwa watoto, kwani ni eneo muhimu ambapo mtoto anajengewa utayari wa shule na kumudu mahiri mbalimbali ikiwemo kusoma, kuandika na kuhesabu (KKK).

slot gacor