Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Taasisi ya Elimu Tanzania

TET NA UCSAF ZASAINI HATI YA USHIRIKIANO UTAOSAIDIA KUKUZA ELIMU NCHINI

Imewekwa: 02 November, 2026
TET NA UCSAF ZASAINI HATI YA USHIRIKIANO UTAOSAIDIA KUKUZA ELIMU NCHINI
Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) na Mfuko wa  Mawasiliano kwa Wote (UCSAF)  leo tarehe 23/101/2026 katika makao makuu ya ofisi za TET jijini Dar es salaam, zimesaini  hati ya ushirikiano wa mi

Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) na Mfuko wa  Mawasiliano kwa Wote (UCSAF)  leo tarehe 23/101/2026 katika makao makuu ya ofisi za TET jijini Dar es salaam, zimesaini  hati ya ushirikiano wa miaka  mitano katika matumizi ya TEHAMA wenye lengo la kuleta mapinduzi ya kudumu katika ufundishaji na ujifunzaji nchini katika elimu nchini. 

Ushirikiano huo utakuwa kwenye maeneo matatu makuu ambayo ni  Uzalishaji na Uhaulishaji Endelevu wa Maudhui ya Kidijiti (Interactive Multimedia e-Content), Uimarishaji wa Miundombinu ya TEHAMA na Ununuzi wa Seva za Kisasa na Uimarishaji wa Majukwaa ya Usambazaji (Op-school) na TET SomaKwanza TV. 

Akizungumza mara baada ya tukio hilo, Mkurugrnzi Mkuu wa Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) Dkt. Aneth Komba amesema kuwa Ushirikiano huo unatarajiwa kuleta manufaa mbalimbali katika Sekta ya Elimu nchini kwa kuinua ubora wa ufundishaji na ujifunzaji, Kuziba pengo la kidijitali na kijiografia (Bridging the Digital Divide) pamoja na kuimarisha Elimu Jumuishi.

“Kwa kweli ni jambo jema kwa TET kuingia makubaliano ya ushirikiano huu tumetambua kuwa katika enzi hii ya mapinduzi ya kidijitali, Mitaala bora na maudhui ya kisasa ya elimu hayawezi kufikia walengwa wake kikamilifu bila miundombinu imara ya TEHAMA,” amesema Dkt. Komba.

Dkt. Komba ameongeza kuwa ushirikiano huo wa kimkakati na Mfuko wa mawasiliano kwa wote  umekuja wakati mwafaka katika kutekeleza Dira ya Taifa ya Mwaka 2050 na kuwa TET itatasimamia na kuhakikisha kuwa fedha kutoka Mfuko wa Mawasiliano kwa wote  inatumika kwa uadilifu, weledi, uwazi, na kuleta tija iliyokusudiwa. 

Kwa upande wake , Mtendaji Mkuu wa USCAF, Bw. Mulembwa Munaku amesema  kuwa ushirikiano huo ni kielelezo cha dhamira ya dhati ya Serikali ya Awamu ya Sita, inayoongozwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ya kuhakikisha kuwa mageuzi ya TEHAMA na uchumi wa kidijitali yanamgusa kila mtoto wa Kitanzania.

“Tunaendela kutekeleza DIRA 2050 na ili kufikia malengo ya Dira hii  mojawapo ya vichocheo vya mageuzi vimetajwa kuwa mageuzi ya kidijitali (digital transformation)  na kuwa ushirkiano huu utatusaidia katika kuimarisha matumizi ya teknolojia mbalimbali katika ufundishaji na ujifunzaji kwa wnaafunzi nchini,“ amesema Bw.Munaku.

Mradi huo utaanza kwa majaribio  kwa uzalishaji wa maudhui ya vitabu vinne vya vya Kidato cha Tatu ambavyo ni  vya masomo ya Business Studies ,Historia ya Tanzania na Maadili ,English na Hisabati.

slot gacor