Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Taasisi ya Elimu Tanzania

JITOKEZENI KUANDIKA VITABU

Imewekwa: 12 August, 2024
JITOKEZENI KUANDIKA VITABU
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Elimu Tanzania
Waandishi bunifu nchini wameaswa kujitokeza kuandika riwaya na hadithi mbalimbali zitakazoweza kutumika shuleni kama vitabu vya ziada. Rai hiyo imetolewa tarehe 3/8/2024 na Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Elimu Tanzania Dkt. Aneth Komba wakati wa hafla ya uzinduzi wa  kitabu cha riwaya kiitwacho "A TANGLED WEB" kilichoandikwa na mwandishi Eunice Urio, na kuhimiza suala la uandishi na usomaji wa vitabu ili kuongeza ujuzi katika maisha na ujifunzaji.  "Naomba waandishi bunifu nchini mjitokeze kwa wingi kuandika vitabu ili tupate vitabu vya wanafunzi vya ziada katika kujisomea hasa tamaduni zetu za Kitanzania," Alisema Dkt. Komba. Sambamba na hilo Dkt. Komba alimpongeza Bi. Eunice Urio kwa uandishi wa kitabu hicho cha Riwaya na kuwasisitiza waandishi wengine wajitokeze kuandika kwa maslahi ya Watanzania.  Hafla hiyo ya uzunduzi  ilihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa kitaifa pamoja na walimu kutoka maeneo mbalimbali nchini. Akielezea kitabu hicho, Mwandishi Bi. Eunice Urio amesema kitabu hicho kimegusa uhalisia ya maisha ya familia ya Mtanzania na kubeba mafunzo mengi yatayosaidia kuijenga jamii ya Mtanzania.  Ameendelea kuwatia moyo Waandishi wengine kutokata tamaa licha ya uandishi kuwa changamoto za uandaaji wa muda mrefu pamoja na eneo la kutafuta soko la uuzaji wa vitabu hivyo kwani bado mwamko wa watu kujisomea vitabu upo chini.  Sambamba na hilo, Bi. Eunice ameiomba Serikali kuendelea kuwashika mkono waandishi wa vitabu hasa kwenye eneo la mtaji katika uchapaji na masoko, kwani uandishi wa vitabu vyetu utasaidia kutunza utamaduni wa nchi yetu.  
Miaka 50 ya Taasisi ya Elimu Tanzania