WALIMU WA MADARASA YA AWALI KUPATIWA MAFUNZO
Imewekwa: 28th October, 2023
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) Dkt.Aneth Komba leo tarehe 26/10/2023 ameongoza baadhi ya wajumbe wa menejimenti ya TET katika kikao na uongozi wa Shirika la Room to Read kilichofanyika katika ofisi za TET jijini Dar es Salaam kilichokuwa na lengo la kujadiliana uwezeshaji wa utoaji wa mafunzo ya walimu wa madarasa ya awali nchini.
Kwa upande wa Room to Read waliongozwa na Mkurugenzi Mkaazi wa shirika hilo Bw. Juvenalius Kuruletera akiambata na Afisa Progamu Mkuu Bi.Hether Simpson ambapo kwa pamoja na TET wamekubaliana kuongeza maeneo ya ushirikiano na hasa katika utekelezaji wa Mtaala mpya. Pia Room to Read imekuwa ikishirikiana na TET katika maeneo mbalimbali ya kielimu ikiwemo uandishi wa vitabu na maboresho ya Mitaala.