Karibu

Dkt. Aneth Komba
Mkurugenzi Mkuu
Kwa niaba ya Baraza, Menejimenti na Watumishi wa Taasisi ya Elimu Tanzania (TET), ninawakaribisha katika tovuti hii iliyoandaliwa kwa lengo la kuuhabarisha umma na wadau mbalimbali wa elimu kuhusu shughuli zinazofanywa na TET katika ngazi ya elimu ya awali, msingi, sekondari na ualimu. Shughuli za TET zimegawanywa katika makundi makuu manne ambayo ni:
- kuandaa na kuboresha mitaala,
- kuandaa vifaa saidizi vya kutekeleza mitaala na kuthibiti viwango vya ubora wa vifaa hivyo,
- kutoa mafunzo endelevu kazini kwa walimu na wasimamizi wa utekelezaji wa mitaala na
- kufanya tafiti za kielimu.
Ni imani yangu kuwa tovuti hii itakuwa ni nyenzo muhimu itakayoiwezesha jamii kupata habari sahihi zilizomo kwenye taarifa, machapisho, nyaraka na miongozo mbalimbali. Natoa wito kwa wadau wote kuendelea kuvinjari tovuti hii na kwa kadri itakavyohitajika kuwasiliana nasi kwa maoni, ushauri au ufafanuzi zaidi kuhusu huduma zetu.
Dr. Aneth Komba
MKURUGENZI MKUU