VIGEZO VYA KUSHIRIKI DURU YA NNE YA TUZO YA TAIFA YA MWL. NYERERE YA UANDISHI BUNIFU VYATAJWA

Mwenyekiti wa Tuzo ya Taifa ya Mwalimu Nyerere ya Uandishi Bunifu Prof. Penina Mlama akiwa katika ofisi za TET Jijini Dar es Salaam leo Agosti 13, 2025 ametaja vigezo vya jumla vya kushiriki katika duru ya nne ya shindano la tuzo hiyo ambayo kilele chake huwa Aprili 13 kila mwaka.
Vigezo hivyo ni kama ifuatavyo:
1. Mshiriki awe raia wa Tanzania.
2. Andiko bunifu liwe katika lugha ya Kiswahili.
3. Sehemu yoyote ya mswada isiwe imechapishwa na mchapishaji au kuchapishwa binafsi pamoja na kuchapishwa mtandaoni na magazetini, au kurushwa katika vyombo vya habari na burudani au kuoneshwa jukwaani.
4. Mwandishi anaruhusiwa kushiriki andiko bunifu moja tu katika nyanja atakayochagua.
5. Mswada utakaoshinda tuzo nyingine hautazingatiwa.
6. Andiko bunifu litakalowasilishwa liwe andiko makini lililojikita katika masuala muhimu ya jamii.
7. Miswada iliyoshika nafasi ya 1 - 10 katika tuzo ya miaka iliyopita haitaruhusiwa kushiriki. Hata hivyo, mwandishi anaweza kuleta mswada mwingine.