Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Taasisi ya Elimu Tanzania

TUZO YA TAIFA YA MWL. NYERERE YA UANDISHI BUNIFU KUENDELEA KUCHOCHEA UANDISHI NA USOMAJI NCHINI

Imewekwa: 20 November, 2024
TUZO YA TAIFA YA MWL. NYERERE YA UANDISHI BUNIFU KUENDELEA KUCHOCHEA UANDISHI NA USOMAJI NCHINI
Tuzo ya Taifa ya Mwalimu Nyerere ya Uandishi Bunifu itaendelea kuchochea uandishi na usomaji hapa nchini na kuchangia kukuza lugha ya Kiswahili. Hayo yamesemwa na Waziri wa Elimu, Sayansi
Tuzo ya Taifa ya Mwalimu Nyerere ya Uandishi Bunifu itaendelea kuchochea uandishi na usomaji hapa nchini na kuchangia kukuza lugha ya Kiswahili. Hayo yamesemwa na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda leo tarehe 18/11/2024 jijini Dar es salamaa , wakati wa hafla ya uzinduzi wa ugawaji wa vitabu vilivyoshinda Tuzo hiyo kwa Mwaka 2022/2023 na kimoja cha Tuzo ya Mwaka 2023/2024.  Akieleza kuhusu tuzo hiyo Mhe. Prof. Mkenda amesema kwamba, tuzo hiyo ina lengo jema la kuchochea Watanzania kuweza kuandika vitabu na hapa nchini ili kuweza kukuza eneo la usomaji. "Tuzo hii itaendelea kuchochea waandishi wengi kuandika vitabu vizuri na vyenye maadili ambavyo vitasaidia katika kutumika shuleni kwa watoto wetu na hii itasaidia sana Watanzania wengi kupenda kujisomea vitabu vilivyoandikwa kwa lugha yao ya Kiswahili" amesema Prof.Mkenda"
Miaka 50 ya Taasisi ya Elimu Tanzania