TET YAKABIDHI VIFAA VYA KIELETRONIKI KWA SHULE YA MSINGI TEGETA 'A' NA KIMBIJI SEKONDARI
Imewekwa: 20th April, 2023
Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) tarehe 18 na 19/04/2023 imekabidhi vifaa vya kielektroniki kutoka nchini Korea kupitia mradi wa KLIC 2022 (Korean e-learning
Improvement Cooperation 2022) pamoja na uzinduzi wa maabara ya TEHAMA
kwa shule ya Msingi Tegeta A na Shule ya Sekondari Kimbiji za jijini Dar es salaam.
KLIC 2022 ni programu ya mafunzo yaliyotolewa na
nchi ya Korea kwa kushirikiana na Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) kwa njia
ya mtandao kwa walimu 40 wa shule ya msingi Tegeta
A na Shule ya Sekondari Kimbiji.
Akikabidhi vifaa hivyo, Mkurugenzi Mkuu wa TET Dkt. Aneth A.Komba amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania,Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuboresha sekta ya Elimu nchini, ambapo ameeleza kuwa walimu katika shule hizo wataweza kutekeleza kwa urahisi kazi ya ufundishaji na
ujifunzaji kwa njia ya kieletroniki.
Dkt. Komba amewataka walimu hao
kuhakikisha wanaleta matokeo chanya ambayo yatasaidia katika uboreshaji wa
elimu.
"Mkayatumie mafunzo vizuri na vifaa hivyo
mlivyokabidhiwa kwa kuleta matokeo chanya na tuone ongezeko la ufaulu kwa
wanafunzi, Amesema Dkt.Komba.
Tukio hilo liliambatana na kukabidhi vishikwambi 40 kwa walimu walioshiriki programu ya mafunzo hayo.