Imewekwa: 04th April, 2023
Mkurugenzi
Mkuu wa Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) Dkt. Aneth Komba amewataka walimu
kuhakikisha wanatumia vitabu vya kiada na ziada vyenye ithibati ya Kamishna wa
Elimu.
Hayo
ameyasema tarehe 03/04/2023 Jijini Dodoma katika ufunguzi wa mafunzo
endelevu ya walimu kazini ya Elimu ya Awali (Watoto Wetu Tunu Yetu) kwa Walimu
na Viongozi wa Elimu yanayotelewa na Shirika la "Children in
Crossfire"
"Walimu
ni chachu ya mabadiliko katika Elimu hivyo nawasisitiza matumizi ya vitabu vya
kiada na ziada vilivyo na ithibati ya Kamishna wa Elimu, ni muhimu sana kutumia
vitabu hivi kwani kuna vitabu vingi huko mtaani vyenye maudhui ambayo
hayaendeni na tamaduni zetu, nasisitiza kila shule itumie vitabu vyenye
ithibati katika kufundisha na kujifunza" amesema Dkt.Aneth.
Aidha,amewaelekeza
walimu hao kutumia Maktaba mtandao ya TET ambayo ina vitabu vyote vya kiada na
ziada, miongozo, mihtasari na mitaala.Ameeleza kuwa Maktaba hiyo kwa sasa
inapatikana bure kwa mtumiaji mwenye laini ya simu ya Airtel na wapo katika
mchakato wa kuongea na kampuni nyingine za simu ziweze kutoa huduma hiyo bure.
Awali,
alishukuru shirika la Children in Crossfire kupitia mradi wa "Watoto Wetu
Tunu Yetu" kwa kuendelea kuwa wadau muhimu katika elimu hususani elmu ya
Awali katika kuboresha mazingira ya ujifunzaji.
Kwa
upande wa Mkurugenzi wa Shirika la "Children in Crossfire" Bwana.Heri
Ayubu amesema kuwa mradi huo wa "Watoto Wetu Tunu Yetu" unatekelezwa
katika mikoa mitatu (Mwanza, Morogoro na Dodoma)
Ukiwa
na lengo la kuendelea kuchangia uboreshaji wa utoaji wa elimu ya Awali nchini
kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa Serikali.
Amesema
kuwa,mwisho wa mradi huo wanatarajia kuona ongezeko kubwa la wanafunzi wenye
utayari wa kuingia darasa la Kwanza.
Mafunzo
hayo yanawashirikisha walimu wa darasa la awali,maafisa elimu,wadhibiti
ubora,maafisa taluma kutoka wilaya za Mpwapwa,
Bahi na Dodoma Jiji.