Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia aipongeza kamati ya Kitaifa ya Maboresho ya Mitaala
Imewekwa: 24th February, 2023
Waziri wa Elimu. Sayansi na Teknolojia Mhe Prof. Adolf Mkenda (Mb), leo tarehe 24.2.2023 amekutana na wajumbe wa Kamati ya Kitaifa ya Maboresho ya Mitaala inayoongozwa na Mwenyekiti wake Prof. Makenya Maboko katika ukumbi wa Mikutano wa Taasisi ya Elimu Tanzani (TET).
Lengo la kikao hicho ilikuwa ni kupokea taarifa ya maendeleo ya kazi ya mapitio ya mitaala ya Elimu ya Awali, Msingi, Sekondari na ualimu. Katika kikao hicho, Mheshimiwa Waziri amepongeza hatua iliyofikiwa na kueleza kuwa amejiridhisha kuwa kamati ipo tayari kufanya wasilisho kwa mamlaka husika juu ya mitaala inayopendekezwa ikiwemo, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan.