Kamati ya Maboresho ya Mitaala yaendelea kupokea Maoni kutoka kwenye Taasisi mbalimbali za kifedha.
Imewekwa: 17th February, 2023
Kamati ya Kitaifa ya wataalamu wa kusimamia maboresho ya mitaala ya elimu ngazi ya Awali, Msingi, Sekondari na Elimu ya Ualimu jana tarehe 16/01/2023 ilipokea maoni na mapendekezo ya Viongozi Wizara ya fedha na Mipango na Taasisi mbalimbali zinazosimamiwa na wizara hiyo juu ya kuingizwa maswala ya fedha katika mitaala ya elimu.
Kikao hicho kimefanyika kwenye ukumbi wa Mikutano- TET jijini Dar es salaam mbali na kuongozwa na Mwenyekiti wa Kamati Prof. Makenya Maboko na pia Wajumbe wa kamati ya maboresho ya mitaala., Mkurugenzi Mkuu wa TET, Wajumbe kutoka wizara ya fedha na mipango, Benki kuu ya tanzania, Tume ya maendeleo ya ushirika Tanzania, Mamlaka ya usimamizi wa Bima, Kitengo cha fedha, Umoja wa mabenki Tanzania, Mamlaka ya masoko ya mitaji na dhamana na Shirikisho la Asasi zinazotoa huduma ndogo za fedha nao walihudhuria.