Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Taasisi ya Elimu Tanzania

TET YAUNGA MKONO JUHUDI ZA DKT. SAMIA ZA KUTEKELEZA MKAKATI WA KKK.

Imewekwa: 26 October, 2026
TET YAUNGA MKONO JUHUDI ZA DKT. SAMIA ZA KUTEKELEZA MKAKATI WA KKK.
TAASISI ya Elimu Tanzania (TET) inaendelea kuunga mkono juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan za kutokomeza changamoto ya Kusoma, Kuandika na Kuhesab

TAASISI ya Elimu Tanzania (TET) inaendelea kuunga mkono juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan za kutokomeza changamoto ya Kusoma, Kuandika na Kuhesabu kwa watoto kupitia mkakati wa KKK uliozinduliwa mapema mwaka 2025.

Juhudi hizo zimefanyika kupitia ugawaji wa vibao vya kielektroniki (electric pads) zaidi ya 50 katika shule ya Msingi Kikundi iliyopo Mkoani Morogoro, vitavyosaidia ujifunzaji na ufundishaji kwa watoto wa Elimu ya awali.

Akigawa vibao hivyo Oktoba 23, 2026, Mkurugenzi Mkuu wa TET Dkt. Aneth Komba alisema, lengo kubwa la ugawaji vibao hivyo ni kuhakikisha, hakuna mtoto anayefika darasa la tatu bila kujua kuandika na kuhesabu (KKK).

"Tunakumbuka kwamba mkakati huu, uliozinduliwa na Mhe. Rais na lengo kubwa la mkakati huu ni kuhakikisha kwamba hakuna mtoto anayefika darasa la tatu, akiwa hawezi kusoma, kuandika na kuhesabu, " alisema Dkt. Komba. 

Alieendelea kusisitiza, "TET imefika na kutoa vibao vya kielektroniki kwaajili ya watoto wa darasa la Awali na la Kwanza kwaajili ya kutumia katika kujifunza kusoma, kuandika na kuhesabu."

Aidha, Dkt. Komba alitoa wito kuwa vifaa hivyo vitumike ipasavyo ili kuweza kufikia lengo la kuondoa tatizo la kusoma, kuandika na kuhesabu kwa watoto wa Awali na darasa la Kwanza.

Kwa upande wake Muu wa shule ya Msingi Kikundi Mwl. Stephen Shekihondo aliishukuru Serikali inayoongozwa na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuunga mkono juhudi za shule ya Msingi Kikundi katika ujifunzaji na ufundishaji hasa kwenye eneo la KKK.

slot gacor