Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Taasisi ya Elimu Tanzania

TET NA WEMA ZAJADILI MABORESHO YA ELIMU NCHINI

Imewekwa: 29 July, 2026
TET NA WEMA ZAJADILI MABORESHO YA ELIMU NCHINI
Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Elimu Zanzibar zimekutana kujadili namna zitashirikiana katika kuboresha Elimu nchini, kupitia mafunzo ya Ualimu na maboresho

Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Elimu Zanzibar zimekutana kujadili namna zitashirikiana katika kuboresha Elimu nchini, kupitia mafunzo ya Ualimu na maboresho ya Mtaala yaliyofanyika. 

Kikao hicho cha kubadilishana uzoefu kimefanyika leo Julai 21, 2026 katika ofisi za TET makao makuu Jijini Dar es Salaam na kuongozwa na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ualimu Zanzibar Bw. Amos John Henock aliyeambatana na maafisa mbalimbali kutoka Wizara hiyo na Mkurugenzi Mkuu wa TET Dkt. Aneth Komba aliyeambatana na menejimenti ya taasisi hiyo. 

Katika majadiliano hayo kwa pamoja wamekubaliana kuendeleza ushirikiano baina ya taasisi hizo katika maeneo mbalimbali ikiwemo katika matumizi teknolojia za elimu na eneo la mafunzo ya ualimu ili kuboresha Elimu nchini Tanzania. 

Akiongoza majadiliano hayo, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Elimu Zanzibar Bw. Amos John Henock ameipongeza TET kwa namna inaendelea kutekeleza Mtaala ulioboreshwa nchini pamoja na mafunzo ya kwa walimu ili kuhakikisha wanatekeleza Mtaala huo kwa ufanisi unaostahili.

Nae, Mkurugenzi Mkuu wa TET Dkt. Aneth Komba amesema, TET inamajukumu ya kuandaa Mitaala, kuandaa vifaa vya kujifunzia na kufundishia kama vile vitabu vya kiada, moduli na mwongozo wa walimu,  kutoa mafunzo kwa walimu na kufanya utafiti na kutoa ushauri wa kitaalamu kwa Serikali na wadau mbalimbali. 

Sambamba na hilo, amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kutoa fedha kwaajili ya utekelezaji wa majukumu ya TET ili kusaidia kukuza ubora wa elimu nchini.

slot gacor