PAZIA LA TUZO YA TAIFA YA MWALIMU NYERERE YA UANDISHI BUNIFU LAFUNGULIWA RASMI
Mwenyekiti wa Kamati ya Kitaifa ya Tuzo ya Taifa ya Mwalimu Nyerere ya Uandishi Bunifu Prof. Penina Mlama amesema dirisha la kuwasilisha miswada ya kazi za ubunifu kwa ajili ya kushindania tuzo hiyo limefunguliwa rasmi leo, Agosti 19, 2026, na litafungwa Novemba 30, mwaka huu.
Kwa mujibu wa mwenyekiti huyo, waandishi bunifu wanatakiwa kutumia kipindi cha takribani miezi mitatu kuwasilisha miswada yao, huku akieleza kuwa matangazo yenye vigezo na taratibu za kushiriki yatatolewa kupitia mitandao ya kijamii ya tuzo hiyo, ikiwemo Instagram, X na Facebook, pamoja na mitandao ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia na Taasisi ya Elimu Tanzania.
Amesema mshiriki anatakiwa kuwa raia wa Tanzania, kazi yake iwe imeandikwa kwa Kiswahili na kila mwandishi anaruhusiwa kuwasilisha andiko moja tu katika nyanja atakayochagua.
Aidha, ameongeza kuwa mswada unaowasilishwa unatakiwa kuwa haujawahi kuchapishwa, iwe kwa njia ya uchapishaji wa kawaida, mitandaoni, magazetini au kupitia vyombo vingine vya habari na burudani.
“Wakati wa kuwasilisha mswada, mwandishi atatakiwa kusaini tamko maalumu kuthibitisha kuwa kazi aliyoleta ni yake na haijawahi kuchapishwa mahali popote,” amesema Prof. Mlama.
Amebainisha kuwa miswada iliyowahi kushika nafasi ya kwanza hadi ya 10 katika miaka iliyopita haitaruhusiwa kuwasilishwa tena, ingawa waandishi waliowahi kushika nafasi hizo wanaweza kushiriki kwa kuwasilisha miswada mipys. Pia, miswada iliyowahi kushinda tuzo nyingine haitazingatiwa katika ushindani wa mwaka huu.
Kwa upande wa vigezo mahususi, amesema tamthilia ya jukwaani inapaswa kutumia vionjo vya sanaa za maonyesho za Tanzania, iwe na muda wa dakika 40 hadi 60, isiwe na maonyesho zaidi ya sita na iwe na wahusika wasiozidi sita. Kwa ushairi, mswada unatakiwa kuwa na mashairi yasiyopungua 50 wala kuzidi 60, huku kila shairi likiwa na beti zisizozidi 15.
Kwa riwaya, urefu unatakiwa kuwa kati ya maneno 60,000 na 100,000, wakati hadithi za watoto zinatakiwa kuwa na kati ya maneno 250 na 500 kwa hadithi moja. Mwenyekiti huyo amesisitiza