SEKTA YA VITABU INA UTAJIRI MKUBWA WA MAARIFA.
Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Huduma za Maktaba, Dkt. Mboni Ruzegea ambaye amemwakilisha Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mh. Prof. Adolf Mkenda amesema kuwa Sekta ya vitabu imedhihirisha kuwa ina utajiri wa maarifa makubwa nchini.
Amesema hayo leo Novemba 26, 2025 wakati akifunga maonesho 32 ya kimataifa ya vitabu Tanzania yanayoendelea katika viwanja vya Bodi ya Maktaba ya Tanzania iliyopo Posta Jijini Dar es Salaam.
"Sekta ya vitabu ina maarifa makubwa sana ,hakika ni eneo ambalo Watanzania tunapaswa kujivunia hivyo Serikali itaenndelea kutoa kipaumbele kwa maonesho haya ya vitabu ili kuinua kiwango cha usomaji," amesema Dkt. Ruzegea.
Hata hivyo ameeleza kuwa maonesho hayo ya vitabu yataendelea kuwepo na kupewa kipaumbele kikubwa nchini ili kukuza utamaduni wa usomaji kwa wananchi.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Elimu Tanzania ( TET) Dkt Aneth Komba ameeleza kuwa, maonesho hayo yawe endelevu kila mwaka ili kusaidia kuchochea suala la usomaji nchini.
"Natamani sana maonesho haya kwa namna yoyote yawe endelevu kutokana na kuwa itaweza kuchochea usomaji umeshuka kuhamasisha usomaji." Amesema Dkt. Komba.
Naye Mwenyekiti wa Chama cha wachipishaji Tanzania, Bw. Heremes Damin ameelezea umuhimu wa maonesho hayo na kuendelea kuomba Serikali iweze kuweka nguvu ili yaweze kufanyika kila mwaka.
Pia amewashukuru wadau wote walioshiriki katika maonesho hayo yaliyoanza tarehe 21 ,Novemba 2025.