PROF. MKENDA AZINDUA KITABU CHA "A TANGLED WEB "
PROF. MKENDA AZINDUA KITABU CHA "A TANGLED WEB "
Imewekwa: 12 August, 2024

Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda akizindua kitabu cha "A TANGLED WEB " kilichoandikwa na Eunice Urio
PROF. MKENDA AZINDUA KITABU CHA "A TANGLED WEB "
Ahimiza Uandishi na Usomaji wa vitabu ili kuongeza ujuzi na ujifunzaji.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda amezindua kitabu cha riwaya kiitwacho "A TANGLED WEB" kilichoandikwa na mwandishi Eunice Urio, na kuhimiza suala la uandishi na usomaji wa vitabu ili kuongeza ujuzi katika maisha na ujifunzaji.
Ameyasema hayo Agosti 2, 2024 katika kituo cha mikutano ya kimataifa cha Mwl. Julius Nyerere katika hafla ya uzinduzi wa kitabu cha riwaya kinachoitwa "A TANGLED WEB", tukio lililohudhuriwa na viongozi mbalimbali wa kitaifa pamoja na walimu kutoka maeneo mbalimbali nchini.
Sambamba na hilo, Prof. Mkenda alisema, Serikali imeanzisha tuzo ya Taifa ya uandishi Bunifu ya Mwalimu Nyerere inayotolewa kwa waandishi wa kiswahili katika riwaya, ushairi, tamthilia, hadithi za watoto ili kuchochea fani ya uandishi Bunifu itayosaidia mabadiliko katika jamii.
Aidha, Prof. Mkenda alisema, Serikali imetenga fedha kupitia Bodi ya Maktaba ya Tanzania kwaajili ya kununua vitabu, huku akisisitiza fedha nyingine zimetengwa kwaajili ya kununua vitabu vitavyokuwa vimeshinda tuzo ya Taifa ya Mwalimu Nyerere ya uandishi Bunifu ili kuhakikisha waandishi wa vitabu wanapata faida baada ya kuchapisha.
" Tumetenga fedha kupitia Bodi ya Maktaba ya Tanzania kwaajili ya kununua vitabu, vilevile tumetenga fedha kwaajili ya kununua vitabu vitavyokuwa vimeshinda tuzo ya Taifa ya Mwalimu Nyerere ya uandishi Bunifu ili kuhakikisha waandishi wa vitabu wanapata faida baada ya kuchapisha." Alisema.
Sambamba na hilo amempongeza Eunice Urio kwa kuandika kitabu kizuri chenye mafunzo kwa wananchi wa Tanzania, na kumpongeza mchapishaji wa kitabu Bw. Aishi Lema kwa kuendelea kuwainua waandishi wadogo ikiwemo kubeba jukumu la uchapaji wa kitabu cha " A TANGLED WEB " cha mwandishi Eunice Urio.