Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Taasisi ya Elimu Tanzania

KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA ELIMU NA UTAMADUNI YARIDHISHWA NA UTENDAJI WA TET

Imewekwa: 12 March, 2025
KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA ELIMU NA UTAMADUNI YARIDHISHWA NA UTENDAJI WA TET
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Elimu, Utamaduni na Michezo imeridhishwa na jitihada zinazofanywa na Taasisi ya Elimu Tanzania(TET) katika kuhakikisha hali ya upatikanaji wa vitabu inaimarika.

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Elimu, Utamaduni na Michezo imeridhishwa na jitihada zinazofanywa na Taasisi ya Elimu Tanzania(TET) katika kuhakikisha hali ya upatikanaji wa vitabu inaimarika.

Hayo, yamebainishwa na Mwenyekiti wa kamati hiyo Mhe. Husna Sekiboko, ambaye pia ni Mbunge wa Tanga wakati wa ziara yao leo tarehe 15/2/2024 jijini Dar es salaam.

Amesema, Serikali imeweka jitihada kubwa, kwa kuwa na mitambo ya uchapaji wa vitabu inayosaidia kuongeza hali ya upatikanaji wa vitabu nchini kwa wakati wote.

Sambamba na hilo, amebainisha kuwa, mitambo hiyo bado ni midogo hivyo haikidhi mahitaji halisi ya uchapishaji ili kumaliza changamoto ya ucheleweshaji na upungufu wa vitabu.

Aidha, Mhe. Sekiboko amesema, kamati itaendelea kuishauri Serikali kuongeza bajeti ya kutosha ili kuweza kununua mitambo mikubwa zaidi itayosaidia kuleta tija zaidi hivyo kupunguza changamoto ya uchapishaji wa vitabu vya kutosha.

Amesisitiza kuwa, lengo la kamati ni kuona Serikali inafikia adhma ya kuhakikisha mpango wa "kitabu kimoja, mwanafunzi mmoja" unaolenga kukuza stadi za ufundishaji na ujifunzaji nchini.

"Ombi letu na ushauri wetu kwa Serikali ni kwamba, waendelee kuboresha ili angalau malengo ya kuhakikisha kila mwanafunzi wa Kitanzania anakuwa na kitabu chake." Amesema Mhe. Sekiboko.

Miaka 50 ya Taasisi ya Elimu Tanzania