Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Taasisi ya Elimu Tanzania

KILA MWANAFUNZI KUPATA ELIMU YENYE UBORA NCHINI

Imewekwa: 29 July, 2026
KILA MWANAFUNZI KUPATA ELIMU YENYE UBORA NCHINI
Serikali imesema itaendelea kutekeleza Sera ya Elimu katika kuhakikisha kila mwanafunzi nchini anapata elimu iliyo sawa  na yenye ubora. Hayo yamesemwa na Waziri wa Elimu, Sayansi na Tkeno

Serikali imesema itaendelea kutekeleza Sera ya Elimu katika kuhakikisha kila mwanafunzi nchini anapata elimu iliyo sawa  na yenye ubora.


Hayo yamesemwa na Waziri wa Elimu, Sayansi na Tkenolojia, Mhe, Prof. Adolf Mkenda leo tarehe 22/7/2026  katika hafla  ndogo ya kukabidhi vitabu vya elimu ya dini ya Kiisilamu kidato cha Sita  kwa Taasisi ya Kusimamia Ufundishaji wa dini ya Kiisilamu shuleni (TISTA ) kupitia Baraza la  Waisilamu Tanzania (BWAKATA) ambapo amesema kuwa hakuna mwanafunzi atakayekosa elimu yenye ubora.


“Kila mwanafunzi nchini atapata elimu kwa ubora kama wanafunzi wengine  na leo hii tumekabidhi vitabu vya elimu ya dini kwa wanafunzi wa kidato cha sita nina imani kuwa vitatumika sawa sawa na ilivyokusudiwa.


Katika maboresho ya Sera ya Elimu na Mitaala yaliyofanyika mwaka 2023, maoni mbali mbali ya kuanzishwa kwa somo  la elimu ya dini ya Kiisilamu yalitolewa na wadau mbalimbali na baadae kuwezeshwa kwa mchakato wa uandishi wa vitabu hivyo vilivyokabidhiwa kwa  TISTA kupitia Baraza la Waisilamu nchini (BWAKWATA).  Prof. Mkenda ,ameishukuru TET kupitia Mkurugenzi  Mkuu, Dkt.Aneth Komba kwa kuhakikisha kuwa uandishi na uchapaji wa vitabu  wa vitabu unamalizika kwa haraka jambo ambalo litasaidia wanafunzi kuanza kuvitumia shueleni.


Kwa upande wa Mwenyekiti wa TISTA, Bw.Musa Kundecha ameshukuru kwa upatikanaji wa vitabu  amabvyo ameeleza kuwa ni hatua nzuri katika ufundishaji na ujifunzaji wa somo  la dini ya Kiisilamu.


Naye mwakilishi wa Mufti Mkuu wa Tanzania, Naibu Kadhi, Bw. Ali Ngeruko amesema kuwa ni hatua muhimu katika elimu ya wanafunzi katika  dini nakuwa  italeta chachu ya kuendelea kujifunza zaidi huku akiishukuru Serikali kwa jitahada  za uletaji wa vitabu kama ilivyoahidi.


Vitabu hivyo vitagawiwa katika shule zote Tanzania Bara na Visiwani ambapo wanafunzi wanaosoma somo hilo wataweza kufikiwa.

slot gacor