Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Taasisi ya Elimu Tanzania

CHAMA CHA WACHAPISHAJI BINAFSI NA WAANDISHI WA VITABU VYA ZIADA WAPITISHWA KATIKA MFUMO WA USIMAMIZI WA TATHMINI YA VITABU VYA ZIADA (QUALITY ASSURANCE MANAGEMENT SYSTEM (QAMS)

Imewekwa: 29 July, 2026
CHAMA CHA WACHAPISHAJI BINAFSI NA WAANDISHI WA VITABU VYA ZIADA WAPITISHWA KATIKA MFUMO WA USIMAMIZI WA TATHMINI YA VITABU VYA ZIADA (QUALITY ASSURANCE MANAGEMENT SYSTEM (QAMS)
Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) imetoa Elimu ya jinsi ya kutumia mfumo wa quality Assurance Management System (QAMS) kwa kwa chama cha wachapishaji binafsi na waandishi wa vitabu vya ziada nc

Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) imetoa Elimu ya jinsi ya kutumia mfumo wa quality Assurance Management System (QAMS) kwa kwa chama cha wachapishaji binafsi na waandishi wa vitabu vya ziada nchini utaosaidia kuongeza ufanisi katika tathmini ya vitabu vya ziada na kuokoa gharama na muda.

Mafunzo hayo yaliyoandaliwa na kitengo cha TEHAMA kwa kushirikiana na udhibiti ubora yamefanyika leo Julai 23,2026 katika ofisi za TET makao makuu Jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na baadhi ya wachapishaji na waandishi wa vitabu.

Akifungua mafunzo mafunzo hayo Mkurugenzi Mkuu wa TET Dkt. Aneth Komba amesema, mfumo huo unaenda kuwa suluhu ya kuokoa muda uliokuwa ukitumika na waandishi wa vitabu na wachapishaji kuja TET, hivyo kila kitu kitafanyika kwa njia ya mfumo.

Pia, Dkt Komba ameeleza, mfumo wa QAMS utasaidia kupunguza gharama ambayo ilikuwa ikitumika kabla na utasaidia kuhifadhi mazingira kwani nakala hazitopita kwenye utaratibu wa karatasi tena.

Sambamba na hilo Dkt. Komba amesema, TET itaendelea kushirikiana kwa ukaribu na wachapishaji na waandishi wa vitabu vya ziada nchini ili kuongeza ufanisi katika utendaji kazi, huku akisisitiza TET itaendelea kupokea maboresho ili kuimarisha utendaji kazi wa mfumo huo.

slot gacor