Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Taasisi ya Elimu Tanzania

TET KUENDELEA KUTEKELEZA MAJUKUMU YAKE IPASAVYO

Imewekwa: 19 June, 2025
TET KUENDELEA KUTEKELEZA MAJUKUMU YAKE IPASAVYO
Mwenyekiti wa Baraza la Taasisi ya Elimu Tanzania (TET), Prof. Maulid Mwatawala alisema kuwa TET itaendelea kutekeleza majukumu na maelekezo yote yatakayotolewa na Serikali kuhusiana na masua

Mwenyekiti wa Baraza la Taasisi ya Elimu Tanzania (TET), Prof. Maulid Mwatawala alisema kuwa TET itaendelea kutekeleza majukumu na maelekezo yote yatakayotolewa na Serikali kuhusiana na masuala ya Mitaala nchini pamoja na majukumu yote ya TET ili kuinua elimu nchini.

Prof. Mwatawala aliyasema hayo tarehe 17/6/2025 katika maadhimisho ya miaka 50 ya TET mbele ya mgeni rasmi, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Kassim  ambaye alimuwakilisha , Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.
 

Pia, Prof Mwatawala alimueleza mgeni rasmi kuwa, kutokana na serikali kuendelea kuipa nguvu TET,  TET imeendelea kufanya kazi kwa mafanikio makubwa . Aidha, aliwashukuru watumishi wote wa TET kwa kuendelea kufanya kazi kwa weledi mkubwa na ubunifiu wa hai ya juu.

Miaka 50 ya Taasisi ya Elimu Tanzania