Katibu Mkuu Elimu afungua mafunzo ya ufundishaji Hisabati
Imewekwa: 08th September, 2021
Katibu Mkuu Elimu afungua mafunzo ya ufundishaji Hisabati
Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dkt Leonard Akwilapo amefungua mafunzo ya Wakufunzi, Wanataaluma na Walimu wa Sekondari wa Somo la Hisabati yanayohusu ufundishaji na Ujifunzaji wa somo hilo.
Mafunzo haya yanatolewa na Chuo Kikuu cha Shangai Normal kilichopo nchini China na kusimamiwa na Benki ya Dunia,yameanza tarehe 3 mwezi Septemba mwaka 2021.
Sherehe ya ufunguzi wa mafunzo imefanyika kwa njia ya mtandao (Zoom).
Akifungua mafunzo hayo, Dkt Akwilapo amesema yatasaidia kuwajengea uwezo wanataalama wa Hisabati na yatasaidia sana kuboresha ujifunzaji na ufundishaji wa somo hilo.
Katibu Mkuu huyo amewataka washiriki kufuatilia mafunzo kwa umakini ili baadaye ujuzi watakaoupata uweze kusambazwa kwa walimu na wakufunzi wengine. Vilevile Katibu Mkuu Dkt Akwilapo ameishukuru Benki ya Dunia kwa kufanikisha miradi mbalimbali ya Elimu nchini Tanzania.
Mafunzo hayo yanayofadhiliwa na Mstaafu wa Benki ya Dunia, Dkt Kin Bing Wu, yatatolewa kwa wiki 15 kwa njia ya Zoom na baadaye safari ya Mafunzo ya wiki mbili nchini China katika Chuo Kikuu cha Shanghai Normal. Jumla ya Washiriki 33 wanashiriki mafunzo hayo.