Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Taasisi ya Elimu Tanzania

MABORESHO YA MITAALA YALIYOFANYIKA NI MAELEKEZO YA DKT. SAMIA SULUHU HASSAN

Imewekwa: 17 June, 2025
MABORESHO YA MITAALA YALIYOFANYIKA NI MAELEKEZO YA DKT. SAMIA SULUHU HASSAN
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Elimu Tanzania Dkt. Aneth Komba amesema, maboresho ya Mitaala yaliyofanyika 2023 ni ya sita chini ya uongozi wa Rais wa Awamu ya sita Mh. Dkt Samia Suluhu Hassan

Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Elimu Tanzania Dkt. Aneth Komba amesema, maboresho ya Mitaala yaliyofanyika 2023 ni ya sita chini ya uongozi wa Rais wa Awamu ya sita Mh. Dkt Samia Suluhu Hassani ambaye ndiye aliyeelekeza kufanyika kwa mapitio makubwa ya Mitaala ili kukabiliana na changamoto za ajira kwa vijana, kukuza uzalendo na maadili pamoja na mengine. 

Dkt. Komba amesema hayo leo Juni 17, 2025 katika maadhimisho ya miaka 50 ya TET haliyofanyika katika ofisi za TET Jijini Dar es Salaam, ambapo mgeni rasmi ni Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania aliyemwakilisha Mhe. Rais. Dkt. Samia Suluhu Hassan. 

Amesema, maboresho haya yamelenga kuwa na wahitimu wenye ujuzi wa kujiajiri, kuajiriwa, kumudu maisha ya siku kwa siku na kutatua changamoto zinazomzunguka katika mazingira halisi.

Aidha, Dkt. Komba amesema, utekelezaji wa Mitaala hii iliyoboreshwa ya mwaka 2023 umeanza mwaka 2024 na kwa sasa madarasa yanayotekeleza Mtaala huu ni Elimu ya Awali, Darasa la Kwanza, Darasa la Pili, Darasa la Tatu na Darasa la nne. 

Ameendelea kusema, kidato cha kwanza mkondo wa jumla na kidato cha Pili mkondo wa Amali na mwaka wa Kwanza elimu ya Ualimu ngazi ya diploma.

Sambamba na hilo, amebainisha kuwa, kwa upande wa kidato cha 5, wanafunzi wataanza kutumia Mtaala ulioboreshwa mwezi Julai, 2025. 

Vilevile, Dkt. Komba amesema, katika elimu ya Sekondari kidato cha I-IV Mtaala umekuwa nyumbufu, mwanafunzi anapoingia kidato cha kwanza anachagua kusoma katika mkondo wa amali au wa jumla. 

Mkondo wa amali unalenga kumpa mwanafunzi maarifa, stadi na ujuzi katika fani atayochagua, huku akiweka wazi fani za mkondo wa amali ni ambazo ni pamoja na Uhandisi, TEHAMA, Ukarimu na Utalii, Kilimo na Ufugaji, Sanaa na Maonesho, Muziki, Urembo, Michezo na Ushoni.

Miaka 50 ya Taasisi ya Elimu Tanzania