DKT. KOMBA ABAINISHA ZAWADI KWA WASHINDI WA SHINDANO LA STADI ZA UFUNDISHAJI

Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Elimu Tanzania Dkt. Aneth Komba amebainisha zawadi walizopata washindi wa stadi za ufundishaji kwa walimu wa msingi na sekondari.
Amesema, zawadi zilizotolewa kwa washindi kumi kwa masomo ya Kemia, Fizikia, Bailojia na hisabati ni fedha, ambapo amesema kwa kila somo mshindi wa kwanza atazawadiwa shilingi Milioni nne (4,000,000).
Ameendelea kusema, Mshindi wa Pili shilingi Milioni tatu (3,000,000), Mshindi wa Tatu shilingi Milioni mbili na nusu (2,500,000), Mshindi wa Nne shilingi Milioni mbili (2,000,000) na Mshindi wa Tano hadi wa Kumi shilingi milioni moja (1,000,000).
Aidha, Dkt Komba amesema kazi ya kutathmini video hizi iliongozwa na misingi ya weledi, usiri, na umakini mkubwa ili kutenda haki kwa washiriki wote, huku akieleza kazi hii imeongozwa na vigezo mbalimbali vya tathmini vikiwemo ubora wa video, maudhui kuakisi umahiri lengwa na kuwa na mtiririko mzuri, uwasilishaji wa somo na umahiri wa mwalimu kutumia mbinu shirikishi zinazokuza stadi za karne ya 21 katika ufundishaji.
Pia, Dkt. Komba amesema, video zilitathminiwa na kupewa alama kisha majaji walitafuta wastani kulingana na idadi yao na video zenye alama za
juu ndizo zilizoteuliwa kuendelea na ushindani katika tathmini iliyofuata.