Tatizo la kushindwaa kuona hapa nchini lipo na huenda limekuwa ni changamoto kubwa katika suala la Elimu hapa nchini.
Lakini pamoja na changamoto hiyo kuwepo hapa nchini, ufumbuzi unaweza kupatikana kwa njia yoyote ili mradi kusaidia watu wenye tatizo la kushindwa kuona kuweza kufanya kazi zao ama kujiendeleza kielemu katika ngazi zote za elimu nchini bila shida yoyote ile.
Kwa upande wa wanafunzi hapa nchini ambao wenye shida ya `kuona na kupelekea kushindwa kusoma katika shule mbali mbali nchini ambao wengine wamekuwa wakitumia kifaa nundu chenye maandishi ya kuwezesha kuona. Vifaa hivyo hujulikana kwa jina la mashine ya Breli Pekini ambavyo vimekuwa vinatumuia hadi wakati huu kwa ajili ya wanafunzi wasioweza kuona. Hata hivyo Neema imeshuka hapa nchini ambapo sasa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kupitia Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) hivi karibuni imefanya uzinduzi rasmi wa kifaa kitakachomsaidia Mwanafunzi asiyeona kusoma, kuandika na mchakato mzima wa ujifunzaji, ikishirikiana na Shirika lisilo la Kiserikali la Sense International Tanzania.
Kifaa hicho kinachoitwa Orbit Reader 20,kinaonesha kitafaa sana katika kumsaidia mwanafunzi katika kusoma na kuwa kama wanafunzi wengine wasio na shida ya kuona, jambo ambalo kifaa hiki kitakuwa mkombozi mkubwa sana katika sekta ya elimu kwa wanafunzi wenye shida ya kuona hapa nchini. Idadi ya wanafunzi wenye changamoto ya kuona hapa nchini ni wanafunzi elfu kumi na nane ambao kwa sasa wanatumia kifaa cha zamani cha Breli pekini ili kuweza kusoma na kuwa kama wanafunzi wengine.
Kifaa hicho kilichozinduliwa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia , Dkt. Caroline Nombo alisema watoto wenye mahitaji maalum hapa nchini wanakabiliwa na changamoto katika ujifunzaji, hivyo kupatikana kwa kifaa cha Orbit Reader 20 kutasaidia wanafunzi wasioona kukabiliana na changamoto hiyo .
Naibu Katibu Mkuu alisema pamoja na changamoto hiyo ya kuona , watoto hao wasioona katika shule mbalimbali hapa nchini hawapaswi kuachwa nyuma na teknolojia hiyo." Teknolojia haichagui, hivyo uzinduzi wa kifaa hiki kutawafanya wawe sambasamba na Teknolojia na kuleta matokeo chanya katika sekta ya Elimu hapa nchini," alisema Naibu Dk Nombo.
Katika uzinduzi wa kifaa hicho cha kusaidia wanafunzi wasio na uwezo wa kuona , rais ikatolewa kwa walimu 12 waliopatiwa mafunzo ya utumiaji wa kifaa hicho cha Orbit Reader 20 kuwa chachu katika kufundisha walimu wengine namna ya kutumia kifaa hicho na kuwezesha wanafunzi watakao kitumia kuwa na uelewa unaokusudiwa.
Taasisi ya Elimu ambao ni wadau wa kubwa wa elimu haoa nchini kupitia Mkurugenzi Mkuu wake Dkt. Aneth Komba katika uzinduzi huo alisema kuwa kwa kushrikiana na Taasisi ya Sense International Tanzania waliamua kuchagua shule mbili za Msingi na nne za Sekondari kwa ajili ya kufanya majaribio ya kifaa hicho ambacho wana imani kitawawezesha wanafunzi wenye matatizo ya kuona kuweza kufanya masomo yao bila usumbufu na bughuza yeyote.
Alisema wanafunzi wasioona wa darasa la nne , la tano na sita katika shule za Msingi pamoja na wanafunzi wa kidato cha kwanza, cha pili na cha tatu watapatiwa Orbit Reader 20 ili wazitumie katika kuandika, kusoma na kuwasiliana na hata walimu wasioweza kusoma maandishi ya breli.
Katika uzinduzi huo, Dkt. Aneth alizitaja shule zitakazoshiriki katika mradi huu kuwa ni Shule ya Msingi Uhuru Mchanganyiko iliyopo Ilala, Shule ya Msingi Toangoma, Shule za Sekondari Mpwapwa, Kilosa, Lugoba, na Haile Selasie ya Zanzibar,ambapo alisema kila shule iliyopo katika mradi huo itapatiwa kifaa cha Orbit 20 kimoja kwa kwa kila mwanafunzi
Pia aliongeza kwa kusema ,shule hizo zilizopo kwenye mpango wa vifaa hivyo vya Orbit 20 zitaweza kutembelewa na wataalamu wa shirika la Sense International Tanzania pamoja na Taasisi ya Elimu(TET)katika mwezi huu wa Agosti zoezi litakalofanyika hadi mwezi Desemba mwaka huu ili kutathmini utumiaji wa vifaa hivi saidizi shuleni vilivyotolewa.
Baada ya vifaa hivyo kutumika , itatolewa taarifa kamili ya tathmini mwishoni mwa mwezi Desemba, 2021 ambapo Mkurugenzi huyo alisema TET itazishauri Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar namna ya njia bora ya kutumia kifaa hiki saidizi shuleni na kuongeza kuwa kila mtu mwenye ulemavu anaweza kupata nafasi ya kujifunza na kuishi kama watu wengine.
Amesema kwa sasa wanafunzi wasioona wanatumia maandishi ya nukta nundu (Parkins Breli) kujifunzia ambapo kifaa hiki gharama yake ni kubwa hasa katika utunzaji wake ambapo gharama zake kwa kifaa kimoja ni shilingi milioni moja.
"Orbit Reader 20 ni kifaa chenye gharama nafuu mara mbili ya mashine ya nukta nundu, ina ukubwa wa GB 32 wa kuhifadhi kumbukumbuku," alisema Bi. Naomi.
Aidha, amesema kifaa hiki kitasaidia kupunguza gharama za uchapaji wa vitabu vya nukta nundu vinavvyofanyika mpaka sasa. Sense International imetoa jumla ya Orbit Reader idadi ya 87 kwa shule sita hizo za Tanzania Bara na Zanzibar zitakazofanyiwa ujaribishaji.
© TAASISI YA ELIMU TANZANIA (TET).Haki zote zimehifadhiwa. Disklaima | Mkataba wa Huduma kwa Mteja | Hatimiliki | site map | Maswali yaulizwayo mara kwa mara | Tathmini ya ETLC | Maktaba Mtandao | Kamusi ya LAT | Learning Management System
Imesanifiwa, Imetengenezwa, na Wakala ya Serikali Mtandao (eGA) na Inaendeshwa na TAASISI YA ELIMU TANZANIA (TET)