WALIMU 17000 KUPATIWA MAFUNZO
Imewekwa: 21st February, 2023
Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) kwa kusirikiana na Shirika la misaada ya maendeleo la nchini Marekani (USAID) kupitia mradi wa Jifunze Uelewe wanatoa mafunzo kwa walimu wa shule za Msingi wanaofundisha darasa la Kwanza hadi la nne katika Mikoa ya Morogoro, Iringa, Ruvuma na Mtwara.
Mafunzo hayo yanalenga kukuza Ustawi wa mwanafunzi katika kuwa Darasa Salama, Saidizi na Jumuishi yanafanyika katika Vituo vya Walimu (Teachers Resource Centre).
Katika kufanikisha zoezi hilo la utoaji wa Mafunzo, TET kwa kushirikiana na USAID iliandaa timu ya wawezeshaji ya kitaifa waliojumuisha wakuza mitaala wa TET na Wakufunzi wa vyuo vya ualimu ambao walijengeana uwezo walikutana Mikumi-Morogoro tarehe 12-13/2/2023.
Wawezeshaji hao waliendelea na jukumu la kuwaandaa wawezeshaji ngazi ya mkoa na wilaya kuanzia tarehe 17-18/02/2023 ambayo waliwawezesha maafisa elimu ngazi ya wilaya na manispaaa wathibiti ubora wa shule na walimu mahiri kwa mikoa ya Iringa,Mtwara,Morogoro na Ruvuma.
Baada ya mafunzo hayo viongozi hao walienda kuwawezesha walimu mahiri katika ngazi ya vituo vya walimu kuanzia tarehe 20/2/2023 hadi 03/03/2023 watawezesha walimu 17000 kutoka Halmashauri zote za mikoa minne.