MTAALA ULIOBORESHWA TOLEO LA MWAKA 2023 UNA VIWANGO VYA KIMATAIFA - PROF. NOMBO
Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Carolyne Nombo amesema Mtaala ulioboreshwa ulioanza kutekelezwa Januari 2024 una ulinganifu wa viwango vya kimataifa, hivyo kuwataka walimu kwenda kufundisha somo la biashara ili kuwasaidia wanafunzi kupata mahiri za kimataifa.
Hayo yamesemwa leo tarehe 27/07/2026 na Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Tkenolojia , Prof. Carolyne Nombo wakati akifungua mafunzo ya walimu wa ajira mpya wa somo la Elimu ya Biashara yanayofanyika katika chuo cha Ualimu Morogoro.
"Naomba niwaambie Mitaala tulionayo sasa ni yakimataifa, yaani inaulinganifu na Mitaala mingine ya kimataifa, kwahiyo ni imani yetu kwamba ninyi mtaofundisha somo hili la Biashara mtasaidia wanafunzi wa somo hilo kipata mahiri za kimataifa" Amesema Prof. Nombo
Ameendelea kusema, Serikali chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Dkt. Samia Suluhu Hassan imewezezesha maboresho ya Sera ya Elimu ya mwaka 2014 toleo la mwaka 2023 yaliyopelekea maboresho ya Mitaala yaliyokidhi ubora wa kimataifa na kuzalisha somo hilo la biashara.
Aidha, Prof. Nombo amesema, Serikali inatambua kazi kubwa na nzuri inayofanywa na walimu nchini katika kumjenga mtoto kuanzia ngazi zote ndani na nje ya shule na kuwataka kuiona kazi hiyo ni ya heshima kuifanya.
Pia, ametoa wito kwa walimu wote nchini kuhakikisha wanajiunga katika jumuia za ujifunzaji ili kupata maarifa zaidi yatakayowasaidia kurahisha katika eneo la ufundiushaji ambapo amesema watumie mifumo kama Learning management sytem (LMS) ambayo itawasaidia katika kujiboresha kwenye kazi yao ya ufundishaji.
Naye Mkurugenzi Mkuu wa TET, Dkt. Aneth Komba ameeleza kuwa mafunzo hayo ni muhimu sana kwa walimu wa ajira mpya kuweza kupata maarifa yatakayowasaidia katika eneo la ufundishaji na kuwa litasaidia sana kwa walimu hao kupata ujuzi na maarifa watakayowapa wanafunzi shuleni ambapo wataweza kuhitimu na baadae kuweza kuajiriwa na kujiajiri wenyewe kupitia somo hilo la biashara.
Kwa upande wake , Mwakilishi wa EDUCATE Bw. Neilson Musila amesema wataendelea kushirikiana na Serikali katika kuhakikisha wanaboresha elimu nchini kwa utoaji mafunzo mbalimbali yenye lengo la kuongeza maarifa na ujuzi.
Jumla ya walimu 704 wa somo la Elimu ya Biashara kutoka shule za Serikali na Zisiszo za Serikali wanashiriki mafunzo hayo ambapo mafunzo yaliyopita jumla ya walimu 1965 walipatiwa mafunzo ya aina hayo ambapo yanatolewa na wataalamu kutoka TET pamoja na vyuo vya ulimu.