Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Taasisi ya Elimu Tanzania

MKAONGEZE JUHUDI ZA KUINUA ELIMU KATIKA NCHI ZENU

Imewekwa: 24 September, 2026
MKAONGEZE JUHUDI ZA KUINUA ELIMU KATIKA NCHI ZENU
Makamu rais wa wa vyama vya jumuia za Mitaala barani Afrika (ACA) Dkt.Jackline Onyango amewataka washiriki wote walioshiriki katika kongamano la siku tatu kuhakikisha wanaporudi katika nchi

Makamu  rais wa  wa vyama vya jumuia za Mitaala barani Afrika (ACA) Dkt.Jackline Onyango amewataka washiriki wote walioshiriki katika kongamano la siku tatu kuhakikisha wanaporudi katika nchi zao kuendeleza juhudi za kuinua elimu ili kupata wanafunzi ili kuacha alama njema.

Ameyasema hayo leo tarehe 25/8/2026 katika ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa JNICC jijini Dar es salaam alipofunga kongamano hilo ambapo ameeleza kuwa yote waliyoweza kuyajadili wanapaswa kwenda kutekeleza katika nchi zao ili kuhakikisha elimu inaendelea kuboreka.

"Hakikisheni  mnafanyia kazi yote tuliyoyajadili hapa nawaomba sana mwende katika maeneo yenu mkayafanyie kazi vyema" amesema Dkt. Onyango.

Kwa upande  wake,Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) Dkt.Aneth Komba amewashukuru washiriki wote wa kongamano na kusema kuwa wameweza kubadilisha mawazo na kupeana uzoefu wa elimu ambao kila mmoja ataweza kuyatumia ipasavyo.

Mkutano huo wa sita wa ACA ambao umehudhuriwa na washiriki mbalimbali  kutoka nchi 22 duniani.

slot gacor