Fri,May 24, 2013
  • Decrease font size
  • Default font size
  • Increase font size

Captions should be here ...

Captions should be here ...

Captions should be here ...

Captions should be here ...

Captions should be here ...

PDF Print E-mail

MAJIBU YA MASWALI YAULIZWAYO MARA KWA MARA:

Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) ina jukumu la kubuni, kuendeleza  na  kuboresha mitaala ya shule na vyuo  kuanzia ngazi ya elimu ya awali, msingi, sekondari na vyuo vya ualimu. Katika kutekeleza majukumu yake TET imekuwa ikipokea maoni na mapendekezo mbalimbali ya wadau kuhusu utekelezaji wa mitaala hiyo. Vile vile imekuwa  ikijibu maswali mbalimbali ya wadau wanaohitaji ushauri au kuelimishwa kuhusu masuala ya mitaala na vifaa vya mtaala kama vile mihtasari, vitabu vya kufundishia na kujifunzia  na miongozo.

Majibu ya TET kwa maswali yaulizwayo na wadau wanaotaka kujua kuhusu utaratibu wa matumizi ya vitabu vya fasihi vya somo la Kiswahili na English vinavyotumika katika shule na vyuo vya ualimu ni kama ifuatavyo:

MDAU: Nifanyeje ili kitabu changu  cha fasihi nilichoandika kwa ajili ya shule na vyuo kiweze kuwafikia walengwa?
TET:  Ili kitabu chako kiweze kutumika katika shule na vyuo vya ualimu ni lazima kipitie hatua zifuatazo:

  1. Kipitishwe na kupewa ithibati na EMAC na BAKITA (kwa vitabu vya fasihi vya somo la Kiswahili).
  2. Baada ya kupewa ithibati na EMAC kiwasilishwe kwa Mchapishaji “Publisher”(nakala 10) ili Mchapishaji aweze kukiwasilisha Taasisi       ya  Elimu Tanzania kwa kufanyiwa tathmini pamoja na vitabu vya waandishi wengine kutoka kwa wachapishaji mbalimbali.
  3. TET kwa kutumia jopo lake la  wataalamu kutoka asasi mbalimbali litatathmini kitabu hicho kwa kutumia vigezo maalumu vilivyowekwa.
  4. Baada ya zoezi la tathmini kukamilishwa na jopo la wataalamu, orodha ya vitabu vilivyopendekezwa kutumika shuleni na vyuoni  huwasilishwa kwa Kamishna wa Elimu kwa ajili ya kuidhinishwa na kutoa tamko rasmi la kuanza kutumika kwa vitabu hivyo.

MDAU: Je, wachapishaji  watajuaje kama wanatakiwa kuwasilisha vitabu hivyo Taasisi ya Elimu  Tanzania kwa ajili ya tathmini?
TET:  Muda wa kubadili vitabu  vya Fasihi vinavyotumika shuleni na vyuoni unapowadia, TET huandika barua kwa Chama cha wachapishaji Tanzania(TAPA) kupitia kwa Mwenyekiti wao  ili kuwaarifu wachapishaji wote kuwasilisha vitabu hivyo kwa tarehe zilizopangwa na TET.

MDAU: TET inatoa muda gani kuhakikisha kwamba wachapishaji wanawasilisha vitabu vyao kwa kuzingatia muda?
TET:  Wachapishaji hupewa muda usiopungua miezi mitatu ili kuweza kukamilisha zoezi hilo  ipasavyo.

MDAU: Je, mchakato wa tathmini ya vitabu vya Fasihi  huchukua muda gani hadi kupendekeza orodha inayopelekwa kwa Kamishana wa Elimu?
TET:   Mchakato wa tathmini hufanyika kwa muda usiopungua miezi sita kwa kuwa jopo la wataalamu hupewa miezi miwili kuvisoma na kuvihakiki kwa kina vitabu hivyo. Baada ya jopo la awamu ya kwanza kukamilisha kazi yake, jopo la awamu ya pili hupitia tena na kuhakiki maoni ya jopo la awamu ya kwanza ili kukamilisha zoezi la uhakiki.

MDAU: Je, mwandishi atapataje taarifa kuwa kitabu chake kimeteuliwa au hakikuteuliwa?
TET:   Baada ya Kamishana wa Elimu kutoa  orodha ya vitabu   vitakavyotumika katika shule na vyuo, orodha hiyo huonesha jina la kitabu, mwandishi na mchapishaji wa kitabu husika. Aidha TET huandika barua kwa wachapishaji wote ambao waliwasilisha vitabu vyao na matokeo ya tathmini. Pia huwajulisha wachapishaji wa vitabu ambavyo vimeteuliwa ili kuhakikisha kwamba vitabu hivyo vinatolewa kwa kukidhi mahitaji ya shule na vyuo   vya ualimu nchi nzima.

MDAU: Je, vitabu vya Fasihi vya somo la Kiswahili na English hutumika muda gani katika shule na vyuo hadi kubadilishwa na kuteuliwa orodha nyingine?
TET:     Vitabu teule  vya Fasihi vinapaswa kutumika kwa muda wa miaka mitatu. Uzoefu unaonesha kwamba wakati wa kutathmini vitabu vipya vinavyotakiwa kubadili orodha ya awali, vilivyo vingi havikidhi mahitaji kama vile kukosa ithibati ya EMAC na kutokidhi mahitaji ya walengwa. Kwa sababu hiyo baadhi ya vitabu hulazimika kuendelea  kutumika hadi vitakapopatikana vitabu vinavyokidhi mahitaji.

Simu:  255-22- 2773005. Nukushi: 255-22- 2774420 Barua pepe:    This e-mail address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it

Last Updated on Tuesday, 17 July 2012 08:16
 

Director General's Desk

Dr. Leonard Akwilapo has been appointed to be the Acting Director General of TIE
Read more
TIE to participate in a Joint "Learning in Secondary Schools Support Initiative"
Read more

News and Events

PostGraduate Diploma in Curriculum Design and Development Programme for the year 2013/14.

Read More


PostGraduate Diploma in Curriculum Design and Development Programme for the year 2013/14 application form.

Apply online


PostGraduate Diploma in Curriculum Design and Development Programme.

Get brochure here


Launching of TIE books writing Project

Read More


Tangazo kuhusu punguzo la bei ya vitabu vya MEMKWA

Maelezo Zaidi


Visitors Counter

037355
Today176
This Week1095
This Month4106

Who is Online

We have 2 guests online

Thank you for Visiting Tanzania Institute of Education (TIE) Website. We would like to hear how did you come to know (TIE) ?
 

Go up